Mashindano ya uandishi kwa Kiswahili ya Mozilla Common Voice

Tukitafakari lugha yetu, Kiswahili, mtazamo wetu ni kuwa ni lugha yenye nguvu na uwezo wa kuendeleza mazungumzo baina ya lugha zingine asilia barani Afrika bila kupatanishwa na lugha za kigeni. Kukubalika kwake pia kama lugha rasmi na Umoja wa Afrika na nchi zingine bali na Afrika Mashariki kufanya mikakati ya kufuata mkondo huu wa kuitumia rasmi  rasmi, nafasi yake imepata nguvu sana.

Kiswahili, kulingana na UNESCO, “ni miongoni mwa lugha kumi ambazo zinawazungumzaji wengi zaidi duniani ikiwa na wazungumzaji milioni 200,” na hili ni jambo linalofaa kuwapa motisha wanaharakati wa lugha na waandishi wa Kiswahili kuandaa kazi kutosholeza mahitaji ya hadhira hii ya wazungumzaji milioni 200.

Tukusubiria saba-saba mwaka huu (ambayo kwa tarekhe ya Kenya huwa ina mandhari ya kisiasa) kwa furaha ya kuadhimisha siku kuu ya lugha ya Kiswahili duniani, kikundi cha Sanaa na fasihi, Hekaya, kwa kushiriakian na Mozilla Foundation kimeandaa mashindano ya uandishi kwa lugha ya Kiswahili. Azimio ni kuvutia mazungumzo zaidi na kupata michango ya sentensi na sauti za Kiswahili mahususi katika jukwaa la Common Voice.

Ombi la kuwasilisha halina mada teule ili kuwapa wawasilishaji uhuru wa kuwa wabinifu bila kizuizi. Pia, mtu yeyote anaweza kuwasilisha kazi yake, sio tu waandishi wa kutokea pwani ya Afrika Mashariki. Itakuwa jambo la kupendeza kusoma kazi kutoka sehemu ambapo Kiswahili hakizungumzwi kama lugha rasmi. Pia, itafurahisha sana kuona kazi, sio tu kwa Kiswahili sanifu, bali kwa lahaja ambazo pia zafaa kupewa umuhimu zaidi.

Wawailishaji wanaweza kuzingatia mada hizi pia:

  • Mziki/nyimbo, densi na vyombo vya kitamaduni.
  • Lugha
  • Tamaduni na turathi.
  • Urembo na mapambo
  • Ujenzi
  • Tiba asilia
  • Fasihi na lugha
  • Utamaduni/mbinu za kutafuta riziki za kitamaduni, k.m ufinyanzi
  • Mambo yanayoathiri jamii kama vile haki za ardhi, makaburi ya wingi , Ukristo na athari yake kwa desturi za kitamaduni.
  • Watu mashuhuri
  • Historia na akiolojia.

Maelekezo kuhusu uwasilishaji:

  • Kazi zitakazowasilishwa zitakuwa katika public domain. Zitakuwa chini ya Public Domain (CC-0) license.
  • Wawasilishaji lazima watie saini Makubaliano ya Uwasilishaji hapa.
  • kazi iwe maneno 2500 kwa uchache na yasizidi 5,000.
  • kazi itakayopokelewa ni inshaa pekee yake wala sio ushairi.
  • Uainishiaji wa maandishi:
    • Usitumie tarakimu mahala pa maneno, k.m 2021
    • Usitumie maneno ya kufupishwa, k.m “USA” au “ICE” kwa kuwa huenda yakasomwa tofauti na yanavyo tamkwa.
    • Maneno yasiwe ya kuvunja heshima.
    • Maneno yasiwe yenye kuchochea aina yoyote ya unyanyasaji au utumizi mbaya wa kijinsia
    • Maneno yasiwe ya kuendeleza dhulma au maonevu ya kijinsia
    • Maneno yaheshimu anuawai/utofauti za kijinsia, k.m matumizi ya viwakilishi vya kijinsia ifaavyo
    • Maneno yasiwe ya kuchochea vurugu/vitisho vya vurugu
    • Maneno yawasilishwe kidigitali wala sio kwa kuandikwa kwa mkono.
    • Kazi iwe yako mwenyewe.

 

Wasilisha kazi yako kabla tarehe 30 Aprili 2022 kwa editor@hekaya.co.ke.

Washindi kutangazwa tarehe 13 Mei 2022

Common Voice, kiswahili, Mozilla, UNESCO


Hekaya Initiative

Writing the East African Coast.

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

© Hekaya Initiative 2018-2020. All Rights Reserved. Design by Crablinks
%d bloggers like this: