Kutu 1: Filamu
Filamu inaanza kwa kimya kizito, huku mziki wa taharuki ukizindikisha nyuso zenye wasiwasi. Ni wazi kuwa Kuna jambo ambalo limetendekea wahusika na kuzua huzuni.
Hii inadhihirika zaidi pindi “Hell” anapovaa viatu na kutoka, Kisha kakake anamuuliza kama dada yao atapata nafuu. Lazma Kuna jambo zito limetendeka ili kufikia katika hali hii ya kuwa dada amelala kitandani namna hii.
Kule maeneo ya mkutano tunampata kiongozi na mlezi wa vijana (anayejulikana kama “Head”) ambao wanatambulika tu kwa nambari wala sio majina. Nambari hazijafatana kutoka moja hadi nyingine, bali zatofautiana na hili linaipa filamu hii fupi maana ya undani sana hadi kuzua hisia kwamba hii ni “hadithi ndani ya hadithi”, au pengine kama tabaka vile. Ile tabaka iliyo matoni mwetu ni kipande kimoja tu cha hadithi hii ya Kutu.
Iwapo Kuna mhusika nambari 12 katika mkutano, lazima pia kuna nambari kabla, na hapa naona kuwa hii maana ya “hadithi ndani ya hadithi” yadhihirika zaidi. Hadithi tunayokumbana nayo ni ya wahusika waliopo hapa sasa hivi. Je, hili ni kundi au shirika la vijan? Genge la majambazi? Waadhirika wa jambo fulani? Je, wahusika ambao hawako mkutanoni, wameuliwa au wako korokoroni? Ama ni wasaliti? Ama pengine ni waadhiriwa au wahusika katika ghasia za baada ya uchaguzi maanake mazingira ya filamu ni 2008.
Filamu hii imetegemea zaidi ustadi wa waigizaji kuleta maana, sanasana kupitia nyuso, lugha ya kiwiliwili na maneno machache.
Yapendeza sana namna wapiga picha wametumia mandhari ya Pwani ili kubuni mtaa wa Kafi, na mtazamaji anakumbana na nyumba za Uswahilini zenye mabati yaliojaa kutu, na ghorofa moja tu- kando na yenye mkutano unafanyika, na ambayo pia haijakamilika- yaonekana kwa umbali.
Sasa, kwa mtazamo huu na jinsi wahusika wamejivaa, ni dhahiri kuwa maisha yao ni duni na hapa swali ambalo najiuliza ni hili: wahusika ni waadhiriwa wa mandhari yao na nyumba zenye paa za kutu, mpaka hali ikawapelekea kutofaulu kama vile kiongozi wao alivyo wauliza- “mbona tunafeli”? Je, mtazamo wao umeadhirika vipi na mandhari na vipi watabadili hali zao waache “kufeli”?
Pia kutu inaweza kuwa sio kwa mandhari tu, bali kwa mtazamo wa wahusika ambao hawajahusishwa, ambao pengine tutasema wanajitokeza kupitia dhana kwamba hali ya “ulala hoi” ya wahusika waliopo inamaaniaha kuwa kuna mabepari au walio na hali nzuri zaidi, wale ambao wanawahuzunikia wenye maisha duni na kuzingirwa na mabamba yalio jaa kutu.
Filamu haswa kama hii inaibua maswali mengi kuhusu kazi ya vijana na ujana katika jamii, hivi ikiwahimiza wasiwe tu wenye kukaa kimya wakati jamii yahitajia mchango wao
Hii ni filamu fupi tena zuri sana na inamualika mtazamaji kuwa mhusika pia kwa namna ambavyo imeacha huru nafasi za kijihusisha ili kuelewa tabaka tulizotaja hapo awali.
Filamu, Kiswhaili, Mabepari, Uswahili