Kale Ya Washairi Wa Pemba

KSh1,200.00

Kale ya Pemba ni kale ya Waswahili na mazingira yao. Maandiko machache ya Abdulrahman Saggaf Alawy na AliAbdala El Maawy yameonesha mazingira ya watu wa kale na mawazo yao. Kale hiyo si kale ya kabla ya Fumo Liyongo, bali ni kale ya akina Kamange na Sarahani. Kamange na Sarahani, waliingia katika karne ya kumi na tisa na kufariki katika karne ya ishirini. Mashairi yao yalivuma pwani yote ya Afrika Mashariki. Mwandishi Abdulrahman Saggaf Alawy, amefanikiwa kukusanya baadhi tu ya maandiko ambayo yote yameandikwa katika mtindo wa kale wenye kujali bahari ya vina, mizani na kibwagizo cha wazo moja. Kamange alipenda sana kutunga mashairi ya kujitoma, ya ushaha, ya utendaji na ukali wa mapenzi ya wanawake. Sarahani alipenda elimu na kusomesha, kuingia katika falsafa na kutoa mawaidha. Kale Ya Washairi wa Pemba ni mkusanyiko mkubwa wa utajiri wa mashairi yenye kuchanganya lahaja mbalimbali za Kipemba, Kimvita, Kiamu, Kimrima, Kivumba na yametumia pia maneno yenye asili ya Kiarabu yatumikayo katika Kiswahili. Kale Ya Washairi wa Pemba kimehaririwa na Abdilatif Abdalla kutoka Mombasa, mshairi wa Sauti ya Dhiki na mwenye kupendwa sana nchini Tanzania alikoishi miaka mingi akifanya kazi katika Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mashairi ya washairi hawa ni changamoto kubwa kwa wasomi wa Kiswahili wa ushairi kwa upeo wa juu sana wa sanaa na umahiri wa lugha.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Kale Ya Washairi Wa Pemba”

Your email address will not be published. Required fields are marked *