Toleo la Pili ya Common Voice ya Shindano la Uandishi wa Insha ya Kiswahili

Kwa mara nyingine tena, mpango wa Common Voice wa Mozilla na Hekaya Arts Initiative, unawaalika waandishi wa Kiswahili kuwasilisha insha za ubunifu. Zawadi za kushindaniwa kwa insha tatu bora zaidi ni USD $400, $250, na $100 mtawalia.

Waandishi wanahimizwa kupanua ubunifu na uhodari wao wa lugha, ikiwa ni pamoja na kuandika katika lahaja mbalimbali za Kiswahili. Jopo la kukagua pia linakaribisha mawasilisho ya kazi zilizotafsiriwa ikizingatiwa kwamba waandishi asili wamepewa sifa.

Insha hizi zitatumika kueneza mradi wa Mozilla wa Common Voice Kiswahili kwa kukuza data huria za Kiswahili, ili kuwezesha utumizi na ujumuishaji wa lugha za Kiafrika katika ujenzi wa technologia.

Mawasilisho yanapaswa kuwasilishwa hapa; na tarehe ya mwisho ni Jumatano, Oktoba 12, 2022. Washindi watatangazwa na kutuzwa kabla ya mwisho wa kutangaza awamu ya tatu ya mashindano haya mwezi wa Novemba..

Muongozo wa Uwasilishaji

 • Mawasilisho yaliyopokelewa yatakuwa katika kikoa cha umma. Kazi zote zitakazowasilishwa zitakuwa chini ya leseni ya Kikoa cha Umma (CC-0).
 • Mawasilisho yanapaswa kuwa kati ya maneno 2,500 hadi 5,000.

Vigezo vya maandishi

 • Kusiwe na tarakimu katika kazi iliyoandikwa kama vile 2021 badala yake tumia maneno.
 • Vifupisho kama vile “USA” au “ICE” vinapaswa kuepukwa kwa sababu vinaweza kusomwa kwa njia ambayo hailingani na tahajia zao.
 • Maandishi yasitumie lugha ya kudhalilisha
 • Maandishi hayapaswi kukuza aina yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji au vurugu.
 • Maandishi hayapaswi kuendeleza au kuunga mkono unyanyasaji wa kijinsia au upendeleo
 • Maandishi yanapaswa kuheshimu tofauti za kijinsia yaani matumizi ya viwakilishi sahihi
 • Maandishi hayapaswi kueneza vurugu na/au vitisho vya vurugu
 • Maandishi yanapaswa kuwa katika muundo wa dijitali sio kuandikwa kwa mkono
 • Maudhui lazima yawe yako mwenyewe, yasiwe na maudhui yaliyoibwa
 • Kumbuka, maudhui ambayo yataonekana kuwa ya kukera kwa njia yoyote yatakataliwa

Blog post and Photo credit

Hekaya Arts Initiative, kiswahili, Mozilla, Mozilla Foundation


Hekaya Initiative

Writing the East African Coast.

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

© Hekaya Initiative 2018-2020. All Rights Reserved. Design by Crablinks
%d bloggers like this: