Mdudu Mbaya Zaidi

Ifuatayo  ni riwaya ya dada Florence Chanya Mwaita iliyoshinda nafasi ya kwanza katika mashindano iliyowezeshwa na Mozilla Foundation.

Isome riwaya yote hapa Mdudu Mbaya Zaidi

…Kwa upande mwingine, mtu anapoitwa mwanasiasa, na anapokuwa na sifa ya ubinafsi, woga humuondoka kabisa kwenye nafsi yake. Ni kama anakuwa na moyo wa chuma. Bali na kung’olewa jino, Adolf Hitler, dikteta wa Kinazi aliyetawala Ujerumani, na kukochea vita vya pili vya dunia, aliogopa nini? Pol Pot, dikteta aliyetawala Kambodia na kusababisha mauaji ya halaiki alimwogopa nani? Nauliza niambiwe, Rais wa tatu wa Uganda, Idd Amin Dada, alipotaka zaidi madaraka, ni kipi kilichomshitua? Ni kipi kilichomsitisha hatua?

Kuhusu mwandishi

Florence Chanya Mwaita ni mtaalamu wa mawasiliano, mwandishi, mhariri, malenga, na mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Ana shahada ya mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Daystar. Alikuwa mhariri mkuu wa Gazeti la Involvement lenye Jamvi la Kiswahili. Hali kadhalika alitafsiria na kuandikia Etaarifa, pamoja na kutoa mchango wake kwenye ukumbi wa mashairi wa Taifa Leo; miongoni mwa majarida mengine. Ikiwa haandiki, anasoma, la sivyo, anafuma.

 

Feature image credit


Hekaya Initiative

Writing the East African Coast.

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

© Hekaya Initiative 2018-2020. All Rights Reserved. Design by Crablinks
%d bloggers like this: