Mapendi Tungu-nzima

Riwaya hii ya mwandishi Omar Kibulanga ilishinda nafasi ya pili katika awamu ya kwana ya mashindano ya uandishi iliyowezeshwa na Mozilla Foundation.

Kuna mfalme aliuawa.

Mwanawe, aliyerithi taji, alikula yamini kubaini chanzo cha vita viliv’oyaleta mauti yaliyomfarakanisha babake na kiti chake cha enzi. Akamuita Waziri aliyekuwa tayari kuukoboa moyo wake kifuani ili upandikizwe kwenye kifua cha mfalme mahututi kisha yeye, haidhuru, awekewe pera pahala pa moyo wake. Waziri huyo aliyedhihirisha uaminifu
timilifu akapewa jukumu la kwenda kudadisi kuanzia utandu mpaka ukoko wa vita hiv’o viliv’oitetemesha milki yao ya Lamu….

Mapend_i T_ungu-nzima

Kuhusu mwandishi

Omar Kibulanga ni mbunifu anayependa kufanya kazi za Kiswahili kwa ajili ya mapenzi yake kwa lugha hiyo pamoja na utajiri wa turathi za Uswahili. Ana hadithi, mashairi, filamu na makala mbalimbali ambayo yanapatikana hususan kupitia akaunti zake kwenye mitandao kama vile Facebook, Instagram na YouTube – Omar Kibulanga. Aidha mashirika mbalimbali yamefaidi huduma zake, mathalani MNET, Supersport, BBC, Royal Media Services, Nation Media Group pamoja na taasisi kadha za kiserikali nchini Kenya.

TETE SERIES EPISODE 1 – HABIB SWALEH ndio kazi yake ya hivi karibuni. Hii ni filamu ya wasifu wa Habib Swaleh, msomi na mwana-mageuzi wa kipekee aliyevuma kisiwani Lamu nchini Kenya kwa kuchangia pakubwa katika sekta za elimu, sayansi na utamaduni na kuacha athari nzuri zilizoenea katika mwambao wa Afrika Mashariki na kwingineko.


Hekaya Initiative

Writing the East African Coast.

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

© Hekaya Initiative 2018-2020. All Rights Reserved. Design by Crablinks
%d bloggers like this: