Afrolit Sans Frontieres- Kiswahili Version

In a press statement received from Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature,  Afrolit Sans Frontieres will be holding the festival in African languages running from October 26 to November 2 2020, with October 26th slotted for the Kiswahili version.

This is exciting news, especially for Kiswahili writers in the continent and the appreciation of African indigenous languages as (in Prof Ngugi Wa Thion’go’s words) ‘the next frontier for publishing in the continent‘. Hopefully, when all these African languages come together, we should see more translation projects in the near future and more contemporary writers publishing in Kiswahili and other languages beyond English and French.

The first Kiswahili session will be at 1500 hrs Kenyan time between Prof Abdilatif Abdalla and two Mabati-Cornell winners Mohammed Khelef Ghassani and Dotto Rangimoto. Both writers will read from their work.

The second session at 2100 hrsKenyan time will feature Ann Samuel, the first Mabati-Cornell Kiswahili prize winner and Prof Ngugi Wa Thiong’o, both in conversation with Moses Kilolo. Prof will read from his poem in Gikuyu followed by readings of the same in Kiswahili.

Visit our shop to get all Mabati-Cornell Kiswahili prize books with free delivery within Mombasa.

The press statement is as below:

 

Tamasha la Fasihi Mtandaoni, Afrolit Sans Frontières,linalohusisha waandishi Waafrika, lina furaha kutangaza Tamasha la Lugha za Afrika litakaloanza mwezi Oktoba 26 hadi Novemba 2, mwaka huu wa 2020. Ingawa kuna matamasha mengine ya lugha za Afrika, hii itakuwa mara ya kwanza kabisa ambapo Tamasha la Fasihi linazihusisha lugha nyingi za Afrika. Miongoni mwa lugha hizo ni Kiswahili, Kizulu, Kiewe,  Kilingala, Kihausa, Kiamhara, Kiyoruba na Kishona. Zaidi ya hayo, shairi lililoandikwa kwa Kikikuyu na mwandishi mashuhuri duniani, Ngugi Wa Thiong’o, kwa madhumuni ya kumkumbuka na kumuenzi mwandishi mwenziwe mashuhuri, Chinua Achebe, litasomwa pia kwa tafsiri za lugha mbali mbali za Afrika.

Zukiswa Wanner,mwandishi, mchapishaji na mwasisi wa  Afrolit Sans Frontières amesema, “Inasikitisha kwamba waliokata shauri kuandika kwa lugha za Afrika wamekuwa wakitengwa na kupuuzwa nje ya mipaka ya lugha zao ingawa wamethibitisha kuwa ni waandishi bora. Kupitia tamasha hili, tutazipaza sauti zao ili kuwaleta karibu na wasomaji wao. Zaidi ya hili, natumai twaweza kuyaendeleza majadiliano na kuiendeleza fani ya tafsiri ili kuhakikisha kuwa riwaya na maandishi mengine ya kuvutia yaliyoandikwa kwa lugha zetu za asili, yanazifikia jamii zetu katika bara la Afrika na pia kwengineko duniani.”

Profesa Mukoma Wa Ngugi, ambaye pamoja na Dkt. Lizzy Attree ni mwasisi mwenza wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika, na mtayarishaji mshiriki wa Tamasha hili, amesema, “Tamasha hili la kihistoria la waandishi wa lugha za Afrika ladhihirisha kuwa lugha za Afrika zatakiwa zichukue nafasi muhimu kwenye sanaa ya uandishi Afrika. Na kwamba fani ya tafsiri itakuwa ni daraja la kuzikutanisha lugha za Afrika ili zizungumze zenyewe kwa zenyewe.”

Kiswahili: Jumatatu Oktoba 26, 2020

Katika Tamasha hili, Kiswahili kitakuwa na vipindi viwili siku ya Jumatatu, Oktoba 26, 2020, vitakavyopeperushwa moja kwa moja kupitia kurasa za Afrolit Sans Frontieres kwenye mitandao ya Facebook na YouTube; na kwa Twitter ni kupitia  AfrolitSansFro1.

Katika kipindi cha kwanza, kitakachokuwa saa 9 alasiri kwa majira ya Afrika ya Mashariki, Abdilatif Abdalla atazungumza na washindi wawili wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika,washairi Mohammed Khelef Ghassani na Dotto Rangimoto, ambao pia watasoma mashairi yao.

Kwenye kipindi cha pili, kitakachoanza saa tatu usiku kwa majira ya Afrika ya Mashariki, itakuwa ni zamu ya  Ngugi Wa Thiong’o; Anna Samuel, ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika; na Moses Kilolo. Ngugi atasoma shairi lake kwa Kikikuyu, likifuatiwa na wafasiri kusoma tafsiri zao za shairi hilo kwa Kiswahili, Kiewe, Kizulu, Kilingala, Kihausa, Kiamhara, Kiyoruba, Kishona, Kikamba na Kiingereza. Anna Samuel atakuwa anazungumza na Moses Kilolo, na pia kusoma maandishi yake kwa Kiswahili.

Kwa Wahariri

“Tamasha la Afrolit ndilo la kipekee kwa mikutano ya kifasihi ambapo wasomaji…wanaweza kusikia kutoka kwa waandishi, na kuzungumza nao kuhusu maswala ambayo wakati mwengine ni magumu au pengine ni mwiko kuyazungumza.” – New York Times

AfrolitHYPERLINK “https://afrolitsansfrontieres.com/” Sans HYPERLINK “https://afrolitsansfrontieres.com/”Frontières, ni Tamasha la Fasihi la Mtandaoni  kwa waandishi wenye asili ya Afrika, lililoasisiwa na Zukiswa Wanner, baada ya mfumko duniani wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19; Covid-19). Tamasha hili huwa na vipindi viwili kwa siku, kupitia ukurasa wake wa Facebook, ambapo mwandishi huelekezwa na mwendeshaji mazungumzo, ambaye pia huratibu maswali kutoka kwa watazamaji.Mradi huu unaungwa mkono na shirika la Swiss Arts Council Pro Helvetia Johannesburg.

 

Tamasha hili limewajumuisha waandishi wengi ndani na nje ya bara la Afrika, na wakati huo huo likisababisha kuandikwa fasihi kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa na Kireno.Kwa habari zaidi tafadhali tembelea wavuti:

https://afrolitsansfrontieres.com

 

Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika

Madhumuni makuu ya Tuzo hii, iliyoanzishwa mwaka 2014 na Dkt. Lizzy Attree na Dkt. Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani), ni kuthamini uandishi kwa lugha za Afrika, kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Afrika zenyewe kwa zenyewe, na pia kutafsiri maandishi ya lugha nyengine kwa lugha za Afrika.

Tuzo hii inadhaminiwa na kampuni ya Mabati Rolling Mills, Kenya. Kampuni hii ni miongoni mwa kampuni za Safal Group; watengenezaji mabati wakuu barani Afrika na wiliomo katika nchi 11 Afrika Mashariki na Afrika Kusini.

 

 

 

 

African publishing, Afrolit Sans Frontieres, KIswahili Prize, Mabati-Cornell, ngugi wa Thion'go


Hekaya Initiative

Writing the East African Coast.

Enter your email address to subscribe to this blog and receive notifications of new posts by email.

© Hekaya Initiative 2018-2020. All Rights Reserved. Design by Crablinks
%d bloggers like this: