Author Archive

Leah Odungo

Leah Wanyika mzaliwa wa pwani na mwandishi chipukizi wa hadithi za hekaya. Alisomea ualimu katika chuo kikuu cha Moi.

Wanyika Nyikani

“Mama…?” alimaka Wanyika baada ya kuitwa na nyanyake na kuelezewa kuwa mgeni aliyewasili alikuwa mamake mzazi. Jua lilikuwa limewaka sana na ulikuwa ni msimu wake wa  mwezi  wa Januari ambapo jua huwaka bila msamaha. Lilichoma   kila jani, mimea ikakauka, shamba likabaki kavu na udongo kupasuka pasuka na kufanya machimbo makubwa makubwa kama mikorongo nyikani. Mchana huo, Wanyika alikuwa akisanya mizizi ya viazi vitamu angalau yeye na nyanyake wapate chajio. Imekuwa ni siku ya nne sasa kabla ya kupata chakula cha haja cha kujaza matumbo yao. Mara nyingi walikunywa maji ya moto tu ili kudanganya matumbo yao na kulala. Na asubuhi ilipofika mpango ulikuwa ni kusaka vibarua kutoka kwa majirani angalau wapate posho. Haya ndiyo yaliyokuwa maisha ya  Mgange Nyika, wakati wa msimu wa kiangazi. Matajiri walitoa  vibarua aina kwa majirani zao na kuwapa kibaba cha posho kama malipo badala ya ngwenje.

%d bloggers like this: